Breaking News

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUNE/13/2017




Habari za usajili barani ulaya za pamba moto ikiwa ni maandalizi ya kuimarisha vikosi vya klabu mbalimbali barani ulaya .Hizi hapa ni habari za usajili zilizochukua sura mpya leo june ,13,2017.Tiririka nayo hapa 

ALEXIS SANCHEZ KUBAKIA ARSENAL
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, ana wasiwasi kuwa huenda Arsenal wakazuia uhamisho wake kwenda Manchester City, na hivyo kuacha Bayern Munich kuwa kimbilio pekee (Mirror).

ARSENAL YAMTAKA LOCAZETTE 
Arsenal wametakiwa kulipa pauni milioni 55 na pauni milioni 12 za ziada iwapo wanataka kumsajili mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, 26 (Daily Telegraph)

JOHN TERRY
 klabu ya Aston Villa wanataka kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry, 36 (Sky Sports).

ANTONIO GRIEZMANN ASAINI MKATABA MPYA ATLETICO MADRID
Mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa, Antoinne Griezmann, 26, amesaini mkataba kusalia Madrid hadi mwaka 2022, (AS) 

ZLATAN IBRAHIMOVIC  KUHAMIA LA GALAXY
mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 35, ameanza mazungumzo kuhusu kuhamia LA Galaxy ya Marekani (Yahoo).

COUTINHO AWATOA HOFU MASHABIKI WA LIVERPOOL
Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho, 25, naye amesema tetesi zinazomhusisha yeye kuhamia Barcelona 'sio suala jepesi' (Independent), 

DIEGO COASTA KUONDOKA CHELSEA
mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa anajiandaa kuondoka kwa mkopo ili kufanikisha uhamisho wake kwenda Atletico Madrid (Evening Standard).

ANTONIO CONTE
Meneja wa Chelsea amemuambia Cecs Fabregas, 30, kuwa atakuwa katika kikosi chake msimu ujao, huku Nemanja Matic, 28, akiwa na uwezekano mkubwa wa kuuzwa (Daily Express).

LERENZO INSIGNE AHUSISHWA KUJIUNGA CHELSEA
Chelsea huenda wakapanda dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, 26, iwapo Eden Hazard atakwenda Real Madrid (Sun).

KYLE WALKER KUTIMKIA MANCHESTER CITY
Manchester City wanajiandaa kuanza mazungumzo na Tottenham kuhusu usajili wa beki Kyle Walker, 27 (Sky Sports), 

MORATA ANUKIA MANCHESTER UNITED
Alvaro Morata anakaribia kujiunga na Manchester United baada ya wakala wa mchezaji huyo kusema haendi AC Milan (Mirror),.


RIYAD MAHREZ  ATAKIWA JUVENTUS 
Juventus wanataka kumsajili winga kutoka Algeria Riyad Mahrez, 26, anayechezea Leicester City. Tottenham nao wanamtaka mshambuliaji wa Leicester Demarai Gray, 20 (Mirror), 

IVAN PERISIC ATAKIWA MANCHESTER UNITED
mshambuliaji wa Croatia na Inter Milan Ivan Perisic, 28, amesema anataka kuhamia Manchester United (Corriere Dello Sport),pia winga wa Manchester United Adnan Januzaj, 22, anasakwa na Real Sociedad ya Spain kwa pauni milioni 8.8 (TalkSport).

MITROVIC KUONDOKA NEWCASTLE
Mshambuliaji wa Newcastle Aleksandar Mitrovic, 22, amekiri kuwa huenda akaondoka msimu huu iwapo dau zuri litatolewa na Fenerbahce wamehusishwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia (DailyStar)

JAMES RODRIGUEZ KUTIMKIA ENGLAND
Manchester United wamekubaliana 'kimsingi' kumsajili James Rodriguez, lakini mkataba wake na Adidas unamtaka avae jezi namba 10 anayovaa Wayne Rooney ambaye hatma yake Old Trafford bado haijulikani,Pia manchester united wanapata upinzani mkali kutoka kwa mabingwa wa epl wakitaka sain ya mchezaji huyo. (OK Diario).

RENATO SANCHES AITOSA MAN U
Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches atawatosa Manchester United na kusubiri dau kutoka Barcelona (Daily Mail), 

JURGEN KLOPP AMPIGIA SIMU KYLIAN MBAPPE
meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amewasiliana na wakala wa Kylian Mbappe ili kujitosa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 100 (Daily Mail).

MOHAMED SALAH KUTUA LIVERPOOL
Liverpool wanakaribia kukamilisha usajili wa winga kutoka Roma Mohamed Salah (Corriere dello Sport), .


MARCO VERRATTI MAMBO BADO MAGUMU KUTUA BARCELONA
Barcelona watatoa euro milioni 100 kumtaka Marco Verratti,Hata hivyo PSG wamesema mchezaji huyo hauzwi msimu huu wa majira ya joto. (La Gazzetta dello Sport), 



TOLISCO  KUJIUNGA NA MIAMBA YA BUNDASLIGA
Bayern Munich wakikaribia kukubaliana ada ya uhamisho na kiungo wa Lyon Corentin Tolisso (Kicker). 



⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Tetesi nyingine kesho tukijaaliw 

No comments