Breaking News

FACEBOOK KUONESHA LIGI YA UINGEREZA

                             Mkuu wa kitengo cha michezo katika kampuni ya Facebook Deen Reed amesema kuna uwezekano kampuni hiyo ikawasilisha ombi la kutaka kununua haki za kuonyesha moja kwa moja mechi za ligi ya Uingereza, huku uvumi kuhusu hatua hiyo ukitanda.    
Haki za kuonyesha mechi za ligi hiyo zinatarajiwa kupigwa mnada mwaka ujao.
Baadhi ya wataalam wanaamini ni muda tu kabla ya Facebook , Amazon na kampuni nyengine za kidijali kuiga mifano ya BT na SkySport katika kuonyesha mechi hizo.
Alipoulizwa mjini London iwapo Facebook itawasilisha ombi hilo, Reed alisema: Ligi ya Uingereza ni washirika muhimu sana kwetu na tunafanya kazi nao kwa karibu.
''Lakini itakuwa makosa kuzua uvumi kuhusu vile tutakavyoifuatilia fursa hiyo, ni mapema mno''.
Na Alipoulizwa iwapo hatua hiyo inamanisha kuna uwezekano, Reed alisema: Hilo ni jibu tosha.
Baada ya kuzinduliwa mwaka 2004 Facebook imekuwa mtandao maarufu dunia na ulipokea zaidi ya dola bilioni 20 mwaka uliopita mapato mengi yakitoka katika matangazo ya mitandaoni.
Kampuni hiyo ina takriban wateja bilioni 2 kila mwezi na milioni 650 kati yao ni mashabiki wa michezo huku wengine milioni 200 wakiwa katika mtandao wa picha wa Instagram.

No comments