YANGA WAIBUKA NA HII BAADA YA KAMATI YA MASAA 72 KUIPA SIMBA POINTI ZA MEZANI
Baada ya Klabu ya Simba kupewa pointi tatu na mabao matatu na Kamati ya saa 72 ambayo ni Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Tanzania kutokana na rufaa waliyoikata dhidi ya Kagera Sugar ya kumtumia mchezaji Mohammed Fakhi kwenye mchezo baina yao Aprili 2 mwaka huu, mahasimu wao Yanga SC wameibuka nao kudai haki yao dhidi ya African Lyon.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam leo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi
amesema kwamba wanawakumbusha Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji madai yao dhidi ya African Lyon kumchezesha Venance Ludovick wa Mbao FC.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwakumbusha TFF (Shirikisho la Soka Tanzania) kwamba na sisi tuna malalamiko yetu Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji dhidi ya African Lyon kumchezesha Venance Ludovick wa Mbao FC katika mechi baina yetu na wao,”amesema Mkemi.
Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Katika mchezo huo ambao Kagera Sugar walishinda mabao 2-1 Uwanja wa Kaitaba, wanadaiwa kukiuka kanuni kwa kumchezesha Fakhi, beki wa zamani wa Simba akiwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
No comments