Breaking News

PELE. Asema Neymar ni bora zaidi ya Ronaldo

Pele anaamini Neymar anahitaji kujiimarisha kufunga kwa kichwa tu ili kuweza kumfunika mfungaji wa muda wote wa Real Madrid Cristiano Ronaldo
Mfalme wa soka, Mbrazili Pele amedai kuwa nyota wa Barcelona Neymar kiufundi yupo juu yaCristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Mshindi wa mare nne wa tuzo ya Ballon d’Or Ronaldo na hasimu wake wa Barca Lionel
Messi wametawala soka la ulimwengu wa sasa sambamba na upinzani mkubwa baina ya timu hizo mbili za Ligi ya Hispania, La Liga.
Neymar ndiye anayeonekana kuwa karibu kurithi enzi za Ronaldo na Messi – vinara wa kutwaa tuzo ya Ballon d’Or – lakini Mbrazili Pele anaamini Neymar mwenye umri wa miaka 24 anahitaji kujiimarisha zaidi kiwango chake ili kumfunika mfungaji wa muda wote wa Real Madrid Ronaldo.
“Tatizo pekee alilo nalo Neymar ni kufunga magoli ya kichwa. Cristiano si bora zaidi yake,” Pele mshindi wa makombe matatu ya dunia alikiambia chanzo cha Brazili UOL.
“Kiufundi, Neymar ni bora zaidi, lakini Ronaldo ni bora zaidi anapotumia kichwa chake.
“Sijamwona Neymar akifunga kwa kichwa, na hilo ni pungufu [ambalo Ronaldo amemzidi].”
Neymar hajawa hatari mbele ya goli katika kikosi cha mabingwa watetezi wa La Liga Barcelona msimu huu.
Katika mechi 16 alizocheza mhula huu, Neymar amefunga magoli matano, huku akitoa pasi sita za magoli.

Coment.

No comments