KLOPP.liverpool wanatakiwa kuwa wajanja kama chelsea"
Klopp: "Liverpool wanahitaji kuwa wajanja kama Chelsea"
Jurgen Klopp amewahamasisha wachezaji wake kujipanga zaidi na kuwataka kujifunza kwa wenzao Chelsea
Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amewaambia wachezaji wake wawe na ari na kufanya mambo kama wanayofanya Chelsea kwa kuwa wajanja zaidi dimbani.
Miamba hao wa Anfield waliambulia sare ya 1-1 dhidi ya vijana wa Antonio Conte katikati ya juma licha ya kuutawala mchezo kwa muda mwingi zaidi, kwani Chelsea walitumia janja za kitabu kupata pointi moja.
Klopp sasa amekiri kuwa angependa kuwaona wachezaji wake wakitumia mikakati hiyo ikibidi, lakini anatambua kwamba wachezaji wake wasio wazoefu sana hawawezi kuwa thabiti ndani ya usiku mmoja.
“Naam, tunahitaji kuwa wajanja,” alisema Klopp.
“Sina uhakika kama inawezekana kulazimisha jambo kama hili lakini ni vizuri kuwa mjanja katika soka.
“Ujanja ni sehemu ya mchezo.
“Chelsea ni wazoefu zaidi na wakati mwingine ni wajanja au wana akili nyingi, vyovyote ninavyoweza kusema.
“Nadhani tunaweza kuimarika. Lakini hatuwezi kuimarika kila siku katika kila Nyanja.”
No comments