MANUEL NEUER APATA JERAHA LITAKOLO MUEKA NJE HADI JANUARY
Beyern munich yathibisha kuwa golikipa wake namba moja atakaa nje hadi mwakani kutokana na jeraha alopata jana kwenye mazoezi ya kuikabili schalk04. Manuel Neuer ameumia jana kwenye mazoezi ya timu yake ikijiandaa na mchezo wa leo dhidi ya Schalke 04. Daktari wa Bayern Munich amethibitisha kumfanyia upasuaji wa awali mapema leo na ameumia eneo lile lile aliloumia mwishoni mwa msImu uliopita kwenye mchezo wa UEFA dhidi ya Real Madrid ambalo ni kifundo cha mguu wa kulia.
Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema Bayern itaathirika kwa kumkosa Neuer kwa takribani msimu mmoja lakini hawana namna lazima wazingate afya yake kwahiyo ni busara kumwacha apone kabisa.
Nohodha huyo wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 31 amekuwa msaada mkubwa kwa klabu yake hususani kwenye michezo mikubwa
No comments