KOCHA WA YANGA ASEMA HAYA BAADA YA RATIBA LIGI YA VODACOM KUBADILISHWA
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga ametaja kusikitishwa na mabadiliko ya ratiba ya Ligi kuu Tanzania ambayo yamefanywa na bodi ya ligi nchini.
Kocha huyo Mzambia ambae hivi karibuni aliondokewa na Baba yake Mzazi saa kadhaa baada ya kurejea nchini amekutana na mabadiliko ya ratiba ambayo yametokana na upangaji mbovu wa bodi ya ligi ambao haukuzingatia ratiba za FIFA na CAF huku ukizifanya timu kuanza kuvuruga ratiba katika michezo ya pili ya raundi ya kwanza ya ligi hiyo.
"Inasikitisha kuona ratiba ya ligi ikibadilika mara kwa mara,jambo hili lina athari kubwa,tulipanga kusafiri leo kwa ajili ya mchezo wa tarehe 6,lakini sasa tunalazimika kuongeza siku zaidi,hii ina maana kuwa 'program' zote zilizowekwa awali zinavurugika" - George Lwandamina.
Hata hivyo Yanga iliyokua imepangwa kucheza na Njombe mji Fc keshokuta 06/09/2017 baada ya mabadiliko yaliyofanyika kutokana na wiki ya FIFA kuingia, hata hivyo ratiba hiyo imelazimika kupanguliwa twna kutokana na ubovu wa upangaji wa ratiba ya awali hivyo Yanga atacheza na Njombe Mji Fc wikendi hii tarehe 09/09/2017.
No comments