Breaking News

MATIC NA DIEGO COASTA WAACHWA LONDON HUKU KIKOSI HICHO CHA CHELSEA KUELEKEA CHINA KWA AJILI YA MAANDALIZI YAO YA MSIMU

Diego Costa na Nemanja Matic hawamo kwenye Kikosi cha Chelsea ambacho Jumatatu kitaruka kwenda China kuanza Ziara yao ya Matayarisho ya Msimu Mpya huku kukiwa na ripoti kuwa Wachezaji hao watawahama Mabingwa hao wa England.
Meneja wa Chelsea Antonio Conte amewajulisha Wachezaji hao Wawili kuwa hawamo kwenye Msafara.
Straika Diego Costa, Mchezaji wa Kimataifa wa Spain mwenye Umri wa Miaka 28, anataka kurejea Klabu aliyotokea Atletico Madrid licha ya kuwa hataweza kusajiliwa na kucheza hadi Januari Mwakani kwa vile Klabu hiyo inatumikia Kifungo cha FIFA cha Kutosajili Wachezaji Wapya kwa kukiuka Kanuni za Kusajili Wachezaji Chipukizi.
Nae Nemanja Matic, mwenye Miaka 28, anatakiwa na Man United na Klabu kadhaa za Italy huku mwenyewe akitaka kuhama hasa baada ya Chelsea kumsaini Kiungo wa AS Monaco Tiemoue Bakayoko ambae anatarajiwa kumbadili Matic kwenye Kikosi cha Kwanza.
Matic alirejeshwa Chelsea kwa mara ya pili Mwaka 2014 na Jose Mourinho wakati alipokuwa Meneja huko na sasa Mchezaji huyo anatamani sana kuungana tena na Mourinho huko Man United.
Kwenye Ziara yao huko China, Chelsea wataanza kucheza Julai 22 na Arsenal na kisha kuruka kwenda Singapore kucheza na Bayern Munich na Inter Milan
Chelsea - Mechi za Ziara:

22 Julai v Arsenal, Bird’s Nest Stadium, Beijing

25 Julai v Bayern Munich, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

29 Julai v Inter Milan, National Stadium, Singapore (International Champions Cup)

6 Agosti v Arsenal, Wembley Stadium (Community Shield)

No comments