LALIGA MAMBO BADO MAGUMU MADRIDI,BARCA ZAPATA USHINDI MNONO
REAL MADRID Jana waliinyuka Sevilla 4-1 ndani ya Estadio Santiago Bernabeu Jijini Madrid na sasa kuhitaji Pointi 4 tu katika Mechi 2 walizobakiza ili kuwa Mabingwa wa LA LIGA huko Spain kwa mara ya kwanza tangu 2012.
Jana, Mabingwa Watetezi Barcelona, wakicheza Ugenini, waliiwasha Las Palmas 4-1 kwa Bao 3 za Neymar na moja la Luis Suarez na kuendelea kuongoza La Liga wakiwa Pointi sawa na Real na wao wako juu kwa ubora wa Magoli lakini wamebakisha Mechi 1 tu wakati Real wana Mechi 2.
Bao kwenye Mechi ya real na Sevilla zilifungwa na Nacho, Cristiano Ronaldo, Bao 2, na Toni Kroos.
No comments