Breaking News

SIMBA YAPUNGUZWA KASI YA UBINGWA NA TOTO AFRICA YATOKA SARE YA BILA KUFUNGANA




Wenyeji wa Jiji la Mwanza Toto Africans ‘Wanakishamapanda’ wameipunguza kasi Simba katika mbio za ubingwa kwa kutoka sare tasa kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba jijini humo.
Sare tasa hiyo sio ya kushangaza kwa Simba kutokana na historia ya miamba hiyo kwenye klabu hiyo ya Toto, kwa miaka mingi Simba wamekuwa wakipata upinzani mkali kutoka kwa wenyeji hao pindi wanapokanyaga ardhi ya kanda ya Ziwa.
Matokeo hayo yanaipa Simba alama 62 kileleni mwa msimamo wa ligi kuu huku mahasimu wao wakishika nafasi ya pili. Toto inafikisha pointi 26 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 14 ikiishusha Maji Maji nafasi ya 15.
Mwamuzi kutoka Mara Jacob Adongo alichezesha mchezo huo akisaidiwa na Hassan Zani wa Arusha na Abdallah Mkomwa wa Pwani. Kulikuwa na kosa kosa pande zote mbili upande wa Simba raia wa Ivory Coast, Frederick Blagnon akipoteza nafasi ya wazi na kwa Toto, Nahodha Reliant Lusajo Mwakasagule naye akipoteza.

Kipindi cha pili kocha Mcameroon wa Simba, Joseph Omog alianza kwa mabadiliko mfululizo akiwatoa kiungo Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Laudit Mavugo na kuwaingiza kiungo Mwinyi Kazimoto na mshambuliaji Ibrahim Hajib.
Pamoja na mabadiliko hayo, mchezo uliendelea kuwa mgumu na Omog akaamua kumtoa na winga Shiza Kichuya na kumuingiza mshambuliaji Juma Luizio, wakati kocha wa Toto, Furgence Novatus alimtoa Jamal Soud Mtengeta na kumuingiza Hamad Nathaniel Mbumba.

Kikosi cha Toto Africans ; Mwasa Kirungi, Juvenary Pastory, Ramadhani Malima, Hamim Abdul, Yussuf Mlipili, Carlos Kirenge, Jamal Mtengeta/Hamad Mbumba dk75, Hussein Kasanga, Waziri Junior, Reliant Lusajo na Jaffar Mohammed.

Kikosi cha Simba SC ; Daniel Agyei, Janvier Besala Bokungu, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga, Juuko Murshid, James Kotei, Shiza Kichuya/Juma Luizio dk76, Muzamil Yassin, Frederick Blagnon, Laudit Mavugo/Ibrahim Ajib dk58 na Mohammed ‘Mo’ Ibrahim/Mwinyi Kazimoto dk54.

No comments