LOTHAR MATTHAUS:ANAAMINI BAYERN ITACHEZA VIZURI BILA MATS HUMMELS KATIKA MCHEZO WAO DHIDI YA REAL MADRID
Nyota wa zamani wa Bayern Munich Lothar Matthaus amesema klabu yake inaweza kucheza dhidi ya Real Madrid katika mzunguko wa kwanza wa robo fainali Ligi ya Mabingwa barani Ulaya bila uwepo wa Mats Hummels.
Kocha Carlo Ancelloti aliamua kumpumzisha Hummels kwenye mchezo wa Bundesliga dhidi ya Borussia Dortmund wakitoka kifua mbele kwa mabao 4-1 akiwa na jicho la akiba lakini bahati mbaya alipata majeruhi ya kifundo cha mguu katika mazoezi juzi.
Matthaus anasema Bavarians hawana sababu ya kuhofia kumkosa nyota huyo kwani Javier Martinez na Jerome Boateng wana uwezo wa kubeba majukumu sawasawa.
No comments