LUIS SUAREZ:bado nafasi ipo ya kufuzu klabu bingwa ulaya
Mshambuliaji wa Suarez Barcelona amesema kuwa bado hawajakata tamaa ya kufuzu katika robo fainali ya kombe la klabu bingwa Ulaya.
Mabingwa hao watetezi wa hispania walifungwa 4-0 na Paris St- Germain katika mchezo wa kwanza ktk hatua ya mtoano hapo siku ya Jumanne.
Barcelona watawalika PSG ktk hatua ya pili katika uwanja wa Nou Camp tarehe 8 mwezi Machi lakini hakuna timu iliyofanikiwa kupata ushindi baada ya kufungwa magoli manne katika raundi ya mtoano
''Iwapo tunataka kuweka historia katika klabu hii basi tutalazimika kubadilisha matokeo haya alissema mshambuliaji huyo wa Uruguay.Sisi ndio timu bora duniani.Na iwapo kuna timu ambayo inaweza kubadili matokeo haya ni Barcelona''.
Klabu ya Barcelona imeshinda kombe la Ulaya ama lile la vilabu bingwa Ulaya mara tano na wamefanikiwa kufuzu katika robo fainali mara tisa mfululizo.
''Kushindwa tulivyoshindwa ni vigumu na uchungu.Itakuwa vigumu sana lakini changamoto nzuri sana'', aliongezea.
Alipoulizwa kuhusu kocha wa klabu hiyo Luis Enrique ambaye kandarasi yake inakamilika mwishoni mwa msimu huu,Suarez alisema ''sote tunapaswa kulaumiwa''.
''hatukucheza vyema na sote lazima tuchukue jukumu la kushindwa''.
Barcelona ambayo iko katika nafasi ya pili katika msimamowa ligi na pointi moja nyuma ya viongozi Real Madrid wanakabiliana na Legannes pale nou camp majira ya usku leo jumapili
No comments