Kuelekea mchezo kati ya simba na yanga haya hapa mambo 5 yanatarajiwa kutokea ktk mchezo huo
Tayari vijembe na kejeli zimeanza mitaani kuelekea mchezo huu huku kila upande ukijinasibu kuibuka na ushindi siku hiyo kisa ubora wa kikosi chao
Kuna baadhi ya mambo yamekuwa kama desturi sasa kwenye mechi za Simba na Yanga , karibu kila mchezo wamekuwa yakijirudia
Watani wa jadi Simba na Yanga watavaana siku ya Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu, mechi inayotarajiwa kupigwa majira ya saa kumi jioni uwanja wa taifa jijini Dar es salaam
Tayari vijembe na kejeli zimeanza mitaani kuelekea mchezo huu huku kila upande ukijinasibu kuibuka na ushindi siku hiyo kisa ubora wa kikosi chao
Ungana na mwandishi wetu anakuletea mambo matano yanayotarajiwa kutokea kwenye mchezo huo
1. Mfumo wa kielotroniki kuchelewesha mashabiki kuingia kiwanjani
Msimu huu TFF wamekuwa wakitumia mfumo wa kisasa wa kielotroniki kuingia kiwanjani hasa kwenye kiwanja cha Taifa na kile cha Uhuru, ila mfumo huu umekuwa na changamoto nyingi kama kusimama kufanya kazi kutokana na kuzidiwa na idadi ya mechi, hivyo mchezo wa Jumamosi utabiri wa mashine hizi kuchelewesha watu kuingia kiwanjani ni mkubwa kutokana na idadi ya watu siku hiyo huku mashine zikiwa chache
2.Mashabiki wa kila upande kuzimia
Imekuwa kama desturi kwenye mechi za Watani wa jadi kuona kundi kubwa la mashabiki wakidondoka kutokana na hewa, bila shaka hata wikendi hii hali ya mashabiki kudondoka bado itaendelea
3.Simba kumiliki mpira kwa muda mwingi wa mchezo
Katika michezo ya hivi karibuni kati ya Simba na Yanga, Wekundu wa Msimbazi wamekuwa wakitawala katikati kwa muda mwingi wa mchezo, wana wachezaji wa kati wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira kwa asilimia kubwa
4.Tambwe kuifunga Simba kwenye mchezo huo
Mrundi huyu amekuwa kwenye wakati mzuri pindi achezapo na Simba, kuwafunga kwake imekuwa kitu cha kawaida hata siku hiyo wasipo mwekea ulinzi dhabiti bado mshambuliaji huyu atawaadhibu
5.Lawama zote kwa mwamuzi kwa timu itakayofungwa
Mwamuzi wa mchezo huo lazima ataangushiwa zigo la lawama kwa timu itakayo poteza mechi, klabu hizi zimekuwa zikificha udhaifu wao kwa kumsingizia refa kwamba kawaonea
No comments