SOUTHMPTON YAPATA PIGO KUELELKEA MCHEZO WAO DHIDI YA TOTTENHAM
Mshambuljia wa Southmpton Charlie Austin amepigwa marufuku ya mechi tatu na shirika la kandanda la FA kwa kucheza vibaya.
Austin alimpiga kiatu kipa wa Huddersfield Jonas Lossl, usoni wakati wa mechi ya Jumamosi ambapo walitoka sare ya 1-1.
Mfungaji huyo bora wa Southampton mwenye umri wa miaka 28, ambaye amefunga mabao 6 msimu huu atakosa mechi dhidi ya Tottenham, Manchester United na Crystal Palace.
Alipata jeraha na kuondolewe uwanjani dakika ya 79.
Meneja wa Southampton Mauricio Pellegrino alisema kuwa jeraha hilo litamweka nje Austin kwa wiki kadhaa.

Alipata jeraha na kuondolewe uwanjani dakika ya 79.
Meneja wa Southampton Mauricio Pellegrino alisema kuwa jeraha hilo litamweka nje Austin kwa wiki kadhaa.
No comments