UINGEREZA YAPELEKA TIMU SITA(6) DROO YA CHAMPIONI LIGI (CL) ZISOME HAPA CHINI

Mabingwa wa Ligi ya Premia Chelsea, Tottenham waliomaliza wa pili na Manchester City waliomaliza wa tatu wote wamo kwenye droo
Watajumuika pia na washindi wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Manchester United, pamoja na Liverpool waliofuzu kupitia hatua ya muondoano sawa na mabingwa wa ligi ya Scotland Celtic.
Mechi za hatua ya makundi zitaanza
kuchezwa 12-13 Septemba.
Mara ya mwisho wa klabu sita za Uingereza kufika hatua ya makundi ilikuwa mwaka 2007-08 pake klabu za England Manchester United, Chelsea, Liverpool na Arsenal zilifuzu pamoja na klabu za Scotland Celtic na Rangers.
Liverpool wacharaza Hoffenheim ligi ya mabingwa Uefa
United wakiwa na Sir Alex Ferguson walicharaza Avram Grant na vijana wake wa Chelsea kwenye fainali kupitia mikwaju ya penalti.
zingine hizi hapa zilizofuzu kucheza championi ligi
Mabingwa watetezi Real Madrid wamo kwenye chungu nambari moja pamoja na washindi wengine saba wa ligi kubwa za Ulaya - Chelsea, Bayern Munich, Juventus, Benfica, Monaco, Spartak Moscow na Shakhtar Donetsk.
Chungu hatari nambari mbili kina klabu za England Manchester United na Manchester City, pamoja na washindi mara tano Barcelona na Paris St-Germain wenye mchezaji ghali zaidi duniani - Neymar.
Klabu za Ligi ya Premia Tottenham na Liverpool zimo kwenye chungu nambari tatu nao Celtic wamo chungu nambari nne ambacho kina pia mabingwa wa Uholanzi Feyenoord na Leipzig waliomaliza nafasi ya pili Bundesliga.
Mechi zitachezwa kati ya tarehe
Mechi ya kwanza: 12-13 Septemba
Mechi ya pili: 26-27 Septemba
Mechi ya tatu: 17-18 Oktoba
Mechi ya nne: 31 Oktoba-1 Novemba
Mechi ya tano: 21-22 Novemba
Mechi ya sita: 5-6 Desemba
No comments