NEYMAR JR KWENDA KUPINGA KESI YAKE MAHAKAMANI INAYOMKABILI DHIDI YA KLABU YAKE YA ZAMANI BARCELONA
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar amesema kuwa ataenda mahakamani kupinga mashtaka yaliowasilishwa na klabu yake ya zamani Barcelona.
Barcelona inataka Yuro milioni 8.5 za marupurupu iliomlipa mchezaji huyo baada ya kuandikisha mkataba mpya wa miaka mitano miezi tisa kabla ya kuahamia PSG.
Mchezaji huyo wa Brazil alihamia PSG kwa kitita cha £200m kilichovunja rekodi mnamo mwezi Agosti baada kununua kandarasi yake.
''Neymar atawasilisha ombi lake la kujitetea hivi karibuni'' , taarifa ya mchezaji huyo na mawakili wake ilisema.
Neymar pia anaonekana kusema kuwa Barcelona inafaa kumlipa fedha kufuatia hatua yake ya kuondoka badala ya inavyodaiwa na timu hiyo.
Taarifa yake iliongezea: Licha ya marupurupu anayodaiwa katika kandarasi ya 2016, ni muhimu kusema kuwa mchezaji huyo amewasilisha ombi rasmi la kudai fedha zake katika mahakama.
Siku ya Jumanne Barcelona ilitaka kulipwa marupurupu iliomlipa mchezaji huyo baada ya kuandikisha mkataba mpya pamoja na asilimia 10 ya kucheleweshwa kwa malipo hayo.
Klabu hiyo inamtaka mchezaji huyo kurudisha fedha hizo kwa kuwa tayari alikuwa ameandikisha kandarasi mpya.
No comments