RATIBA YA MICHUANO YA KOMBE LA MABARA HII HAPA

HII HAPA TATHMINI KATI YA PORTUGAL VS MEXICO:
Portugal v Mexico – Kundi A
Timu hizi zilikutana mara ya mwisho huko Foxborough, USA, Mwezi Juni 2014 zikijitayarisha na Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 zilizochezwa Brazil na Bruno Alves aliwapa ushindi Portugal kwa Bao la Dakika za Majeruhi.
Wapo Wachezaji Watatu wa Mexico, Raul Jimenez, Miguel Layun na Hector Herrera ambao hucheza Soka lao huko Nchini Portugal
JE WAJUA?
Portugal vs Mexico:
-Hii itakuwa mara ya pili kwa Timu hizi kukutana na mara zote Portugal ndio wameibuka kidedea.
-Wakati Portugal ni mara ya kwanza kushiriki FIFA Kombe la Mabara, kwa Mexico hii ni mara ya 6.
Kwa upande wa Portugal, Kocha Fernando Santos ana matumaini makubwa na Timu yake ambao ni Mabingwa wa Ulaya na hasa kwa kuwa nae Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo, ambae ndio kwanza anatoka kutwaa Taji la Klabu Bingwa Ulaya na Klabu yake Real Madrid.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Portugal: Rui Patricio; Bruno Alves, Jose Fonte, Raphael Guerreiro, Cedric; William Carvalho, Joao Moutinho, Andre Gomes; Nani, Cristiano Ronaldo, Andre Silva
Mexico: Guillermo Ochoa; Carlos Salcedo, Hector Moreno, Nestor Araujo, Miguel Layun; Jonathan Dos Santos, Hector Herrera, Andres Guardado; Carlos Vela, Javier Hernandez, Raul Jimenez
REFA: Nestor Pitana [Argentina]
MAKUNDI:
KUNDI A KUNDI B
Russia (Wenyeji) Cameroon (CAF)
New Zealand (OFC-Oceania Footbal Confederation) Chile (CONMEBOL)
Portugal (UEFA) Australia (AFC)
Mexico (CONCACAF) Germany (Mabingwa Watetezi)
tathmni kati ya Cameroon v Chile
Kundi B
Baada ya kutwaa Copa America mara mbili mfululizo, Chile sasa, kwa mara ya kwanza, wanatinga FIFA Kombe la Mabara wakati kwa Cameroon hii ni mara yao ya 3 tangu 2003.
Kundi hili lina Mabingwa wa Dunia Germany lakini wengine wataona nafasi yao kwani Germany imeacha wazoefu wengi na kuchukua Vijana na hivyo Timu nyingine zitahisi hii ndio nafasi yao.
Lakini Chile watamkosa Kipa wao Claudio Bravo ambae ni Majeruhi ingawa idara ya mashambulizi ina wakali kina Eduardo Vargas na Alexis Sanchez.
JE WAJUA?
Cameroon vs Chile:
-Hii itakuwa Mechi ya pili kati yao baada ya kukutana Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 1998 na kutoka Sare 1-1.
Cameroon ndio wenye Kikosi chenye Chipukizi wengi baada ya Germany kwenye Mashindano haya na wengi wanatarajia kuwa, chini ya Kocha kutoka Belgium Hugo Broos, hawatafanya vyema hasa baada ya kupigwa 4-0 na Colombia katika Mechi yao ya mwisho ya kujipima nguvu.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Cameroon: Fabrice Ondoa; Collins Fai, Adolphe Teikeu, Michael Ngadeu Ngadjui, Jonathan Ngwem; Arnaud Djoum, Sebastien Siani; Jacques Zoua, Benjamin Moukandjo, Christian Bassogog, Vincent Aboubakar.
CHILE: Johnny Herrera; Mauricio Isla, Gary Medel, Gonzalo Jara, Jean Beausejour; Arturo Vidal, Marcelo Diaz, Charles Aranguiz; Jose Fuenzalida, Eduardo Vargas, Alexis Sanchez.
REFA: Damir Skomina (Slovenia)
FIFA KOMBE LA MABARA
Ratiba/Matokeo:
Hatua ya Kwanza
Jumamosi Juni 17
KUNDI A
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Russia 2 New Zealand 0
MICHUANO HII ITAENDELEA LEO JUMAPILI
Jumapili Juni 18
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
1800 Portugal v Mexico
KUNDI B
Spartak Stadium, Moscow
2100 Cameroon v Chile
Jumatatu Juni 19
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
1800 Australia v Germany
Jumatano Juni 21
KUNDI A
Spartak Stadium, Moscow
1800 Russia v Portugal
Fisht Stadium, Sochi
2100 Mexico v New Zealand
Alhamisi Juni 22
KUNDI B
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
1800 Cameroon v Australia
Kazan Arena, Kazan
2100 Germany v Chile
Jumamosi Juni 24
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
1800 Mexico v Russia
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
1800 New Zealand v Portugal
Jumapili Juni 25
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
1800 Germany v Cameroon
Spartak Stadium, Moscow
1800 Chile v Australia
HATUA YA PILI
Nusu Fainali
Jumatano Juni 28
Kazan Arena, Kazan
2100 Mshindi Kundi A v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]
Alhamisi Juni 29
Fisht Stadium, Sochi
2100 Mshindi Kundi B v Mshindi wa Pili Kundi A [NF2]
Mshindi wa 3
Jumapili Julai 2
Spartak Stadium, Moscow
1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2
FAINALI
Jumapili Julai 2
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2
KILALAKHERI KWA TIMU ZOTE ZINAZOSHIRIKI MICHUANO HII YA KOMBE LA MABARA
No comments