PEP GUARDIOLA AKIRI MSIMU BILA TAJI INGEKUWA BARCA AU BEYERNMUNICH ANGEFUKUZWA
MENEJA wa Manchester City Pep Guardiola amesema angefukuzwa kazi na Klabu zake za zamani Barcelona na Bayern Munich kama angemaliza Msimu bila Kombe lolote.
Huu ni Msimu wa kwanza wa Guardiola akiwa na Man City lakini ndio unamalizika bila wao kutwaa Kombe lolote huku pia wakiwa bado kupata uhakika wa kuwemo 4 Bora za EPL, LIGI KUU ENGLAND, na hivyo kucheza UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao huku wakiwa wamebakisha Mechi 2.
Akiwa na City kwenye Msimu wake wa kwanza, Pep Guardiola ameshinda Mechi 31 kati ya 54 akitoka Sare 13 na Kufungwa 10.
Kwenye Makombe, Guardiola na City yake walitolewa nje Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, wakapigwa nje Nusu Fainali ya FA CUP na kwabwagwa Raundi ya 4 ya EFL CUP.
Guardiola ameeleza: "Kama ni Barcelona na Bayern kama hushindi uko nje. Hapa nimepewa nafasi ya pili na ntajaribu kufanya vyema Msimu ujao!"
Guardiola alitua City kumrithi Manuel Pellegrini akitokea Bayern Munich na kabla alikuwa huko Barcelona na sehemu zote alizoa mafanikio makubwa mno.
Hilo liliwafanya Mashabiki wa City kuwa na matumaini makubwa.
Guardiola, mwenye Miaka 46, aliiongoza Barca kutwaa Makombe 14 katika Miaka Minne yakiwemo Mataji Matatu ya La Liga na Ubingwa wa Ulaya mara 2 kati ya 2008 na 2012.
Kisha akajipumzisha Mwaka Mmoja na 2013 kwenda Bayern alikokaa Misimu Mitatu na kila Msimu kubeba Taji la Bundesliga pamoja na German Cup mara 2.
Katika Mechi 2 za Ligi walizobakisha, City wanatakiwa washinde zote ili wajibakize 4 Bora.
Leo City wapo kwao kucheza na West Brom na Jumapili wapo Ugenini kucheza na Watford.
Hatari kubwa kwa City, pamoja na Liverpool, kwa Nafasi zao za 4 Bora ni Timu ya 5 Arsenal ambayo Leo inacheza na Sunderland na kumalizia na Everton.
Tayari Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameanza vita ya mdomo kwa kudai City wana ubwete kwa vile wanacheza na Timu zilizo salama na hivyo hazina motisha lakini Guardiola amemponda.
No comments