MOURINHO AIJIA JUU RATIBA YA EPL KUHUSU RATIBA YAO YA JUMAPILI HUKU TAREHE 24 WANATAKIWA WAKACHEZE FAINALI YA UROPA LIGI
JOSE MOURINHO ameijia juu EPL, LIGI KUU ENGLAND, na kudai popote kwingine Duniani Manchester United ingepewa Siku 1 ya ziada ya kupumzika kabla ya Mechi yao ya Fainali ya UEFA EUROPA LIGI.
Jumapili Man United wapo huko London Uwanja wa Selhurst Park kucheza Mechi yao ya mwisho ya EPL ambayo haina manufaa yeyote kwa Timu zote 2 mbali ya kukamilisha Ratiba na kisha Jumatano wapo huko Sweden kucheza Fainali ya UEFA UROPA LIGI dhidi ya Ajax Amsterdam ambao Ligi yao ya Netherlands ilimalizika Jumapili Mei 14.
Mourinho amedai baada ya Wiki iliyopita Palace kujihakikishia kubaki EPL kwa kuifunga Hull City na wao kuganda Nafasi ya 6 tu basi Mechi hii ingechezwa Jumamosi na si Jumapili ili wao kupata Siku 1 ya ziada ya Mapumziko.
Kutokana na kutopata msaada huo Mourinho ameamua kuchezesha Kikosi kipya kwenye Mechi hiyo Jumapili na Palace.
Akiongea Jana baada ya kutoka 0-0 na Southampton, Mourinho alieleza: "Nchi nyingine yeyote Mechi hii ingekuwa Jumamosi. Sisi ni wa 6, Palace wako salama!"
Mourinho amedai hakuna anaezijali Timu za England huko England na pia kueleza kimzaha: "Natumai Mashabiki watasapoti Kikosi cha Jumapili na kusamehe ugeni wake na kutojiamini. Na pia Big Sam ataonyesha urafiki na kuwa laini kwetu na kumwambia Wilfried Zaha acheze polepole na kumwacha Christian Benteke nyumbani!"
Mourinho amedokeza kuwa kwenye Kikosi cha Jumapili atakuwepo Paul Pogba ambae hajacheza Wiki yote hii baada kufiwa na Baba yake Mzazi.
Ameeleza: "Lakini pia watakuwepo Chipukizi Demetri Mitchell, Scott McTominay, Axel Tuanzebe, Josh Harrop na Zachary Dearnley huku Kipa akiwa Joel Castro Pereira pamoja na Beki Eric Bailly!"
No comments