KIPRE TCHETCHE AZIITA SIMBA NA YANGA KUFANYA MAZUNGUMZO NAO ENDAPO WATAITAJI HUDUMA YAKE
Aliyekuwa Straika wa Azam FC, Kipre Herman Tchetche, amesema licha ya kutofuatwa na timu yoyote kutoka Tanzania, lakini yupo tayari kurejea nchini kujiunga na Simba au Yanga kama timu hizo zitahitaji huduma yake.
Kipre ni miongoni mwa wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa mara kwa mara katika usajili wa klabu ya Yanga, huku baadhi ya vigogo kupendekeza jina la straika huyo anayekipiga katika klabu ya Al- Nahda Al Buraimi ya Oman.
Yanga imefikia hatua ya kumtaja Kipre baada ya straika wao, Donald Ngoma, kugomea uongozi wa klabu hiyo kuongeza mkataba mwingine, huku ikidaiwa kwamba amepata timu Afrika Kusini.
Kipre alisema, kwamba kwa sasa anasubiri msimu umalizike ambapo wanacheza michuano ya kombe la Majesty, baada ya hapo hajajua ataelekea wapi.
Alisema hadi sasa hakuna kiongozi wa timu yoyote kutoka Tanzania aliyempigia simu kumpa taarifa hizo, lakini kama itatokea yupo tayari kurejea na kucheza soka Tanzania.
“Hizo taarifa za Yanga sijazisikia wala kufuata, kwani bado sijajua hatima yangu hadi hapo nitakapomaliza msimu, suala la dau kwa sasa ni siri yangu kwa timu inayonihitaji,” alisema Kipre. KIPRE : Simba na Yanga Njooni Tuongee..!!!
No comments