Breaking News

FIFA YAPITISHA TIMU 9 AFRIKA KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2026 TAZAMA MABADILIKO YA MABARA YOTE HAPA

Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakapoongezwa na kuwa 48 mwaka 2026.
Hatua hiyo iliidhinishwa Jumatano nchini Bahrain.
Bara la Afrika kwa sasa huwa na nafasi tano pekee.
Fifa kuanza kutumia Video michezoni
Taifa la kumi kutoka Afrika litashiriki katika michuano ya muondoano ya kufuzu, itakayoshirikisha nchi sita, kuamua atakayefaidi kutokana na nafasi mbili za ziada.

Baraza la Fifa lilitangaza pendekezo lake la kwanza kuhusu mpango wa kugawa nafasi hizo 48 tarehe 30 Machi.
Huu hapa mgawanyo wa bara husika idadi ya timu zitakazoshiriki fainal hizo

Afrika - 9 kutoka timu za awali 5

Asia - 8 kutoka timu 4 za awali

Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali

Marekani ya Kaskazini, Kati na 
Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali

Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali
Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali







No comments