Breaking News

FA YATANGAZA SHERIA KALI MSIMU UJAO KWA WACHEZAJI WANAOJIANGUSHA KWA KUKUSUDIA

Kuanzia msimu ujao, wachezaji wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza wenye mazoea ya kusaka penalti au mkwaju wa  Penati kupitia udanganyifu watachukuliwa hatua.
Kwenye sheria mpya zilizopitishwa na bodi ya usimamizi leo katika mkutano wake wa kila mwaka, kamati maalum itatathmini video za mechi za wikendi kila jumatatu kuangalia visa vya udanganyifu.
Kamati hiyo itawajumuisha mmoja wa wasimamizi wa mechi, meneja wa zamani na mchezaji wa zamani.
Chelsea mabingwa EPL
Mchezaji atakayepatikana kujirusha akisaka penalti, kupelekea utoaji wa kadi nyekundu au njano, ataadhibiwa kwa kupigwa marufuku na kukosa baadhi za mechi.
Shirikisho la soka nchini Uingereza FA, limefafanua kuwa madhambi hayo yatajulikana kama ''utapeli wa msimamizi wa mechi''.
Mabadiliko hayo mapya yalihitaji uungwaji mkono kutoka ligi kuu ya Premier nchini Uingereza, ligi ya daraja la chini, EFL na muungano wa wachezaji, PFA.
Wakati huo huo, FA imepitisha mabadiliko zaidi yakiwemo kutenga nafasi tatu kwa wanawake ifikapo 2018, kupuguza wanachama wa bodi hadi 10 na kuwashirikisha waanachama kumi na moja zaidi kuonyesha usawa.

No comments