HAJI MANARA AFUNGIWA MIEZI 12 KUTOJIHUSISHA NA MPIRA NA FAIN YA MILIONI 9
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la mpira wa miguu TFF imemsimamisha Mkuu wa Idara ya Habari wa Simba,Haji Manara kutojihusisha na soka kwa miezi 12 na faini ya milioni 9
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msemwa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu.
No comments