Breaking News

LIVERPOOL YALAZIMISHA SARE KWAKE ANFIELD

HAYA NI MACHACHE YALIYOTOKEA JANA MCHEZO KATI YA LIVERPOOL NA CHELSEA:ANFIELD
Liverpool 1-1 Chelsea.
1. KLOPP KIBOKO YA VIGOGO
Jurgen Klopp kabla ya mchezo wa jana dhidi
ya Chelsea kocha huyo alikuwa amepoteza
mchezo mmoja tu kati ya michezo 14 ya
primia aliyocheza dhidi ya timu "vigogo" (Man
Utd, Man City, Chelsea, Spurs, Arsenal) huku
akishinda mara sita na kutoka sare mara
saba. Kwahiyo matokeo ya sare aliyoyapata
dhidi ya Chelsea sio jambo la kushangaza
sana, Klopp na Liver yake wanajua kucheza
dhidi ya vigogo.
2. GEGENPRESSING
Kama kuna jambo lililowalipa Liver kwenye
mchezo huu dhidi ya Chelsea basi ni falsafa
ya Klopp almaarufu “Gegenpressing", falsafa
ambayo inahusisha mashambulizi ya
kushtukiza lakini zaidi sana “kuwapress” timu
pinzani kwenye eneo lao ktk kukaba, na jana
hii iliwavuruga Chelsea kabisa na kushindwa
kucheza mchezo wao. Unaweza kusema “game
plan” ya Klopp ilimlipa.
3. MATIP WA JANA NA LEO.
Ukiachana na Penati aliyosababisha dhidi ya
Costa, kijana Joel Matip kutoka Kameruni
alimpoteza Costa kwenye mchezo wa jana, ktk
safu ya ulinzi ya Liver umakini na namna ya
kuwapanga wenzake ndiyo silaha kubwa ya
Matip, dhidi ya Bournemouth, Swansea na
Southampton Matip alikosekana na mechi
zote hizo Liver alichezea kichapo.
4. COUTINHO NA SAFU YA USHAMBULIAJI YA
LIVER
Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya mwezi
mmoja kutokana na kuumia Coutinho bado
hajarudi kwenye kiwango chake
kinachofahamika na wengi na matokeo yake
safu ya ushambuliaji ya Liver inakosa “meno”
kwenye lango la wapinzani, ukiachana na goli
moja lililofungwa tena na kiungo wa katikati
jana bado safu ya ushambuliaji ya Liver
inakosa makali ya kumaliza mchezo ILA
MANE amerejea.
5. CHELSEA BILA MPIRA.
Kwa Chelsea kukaa kileleni sio kwasababu tu
ya kushinda michezo mingi bali pia
kwasababu ya kuwa bora wakiwa hawana
mpira wakiwa wanakaba, tofauti ya Chelsea
na timu zingine ni namna ambavyo Chelsea
mara nyingi wanaonekana wakiwa na
“confidence” na wako “organized” hata wakiwa
bado wanashambuliwa na dhidi ya Liver jana
alama moja waliyoipata ni kutokana na
utulivu wa Chelsea kwa sehemu kubwa ya
mchezo pamoja na kwamba walishambuliwa
zaidi.
6. ADUI WA CHELSEA NI “PRESSING”
Mfumo pendwa wa 3-4-3 ndani ya Chelsea
huchagizwa zaidi na mashambulizi ya timu
hiyo kuanzia eneo la nyuma hivyo timu
ambayo itaweza “kuwapress” Chelsea kwa
umakini kutoka eneo la Azpilicueta, Luiz na
Cahill basi ni dhahiri Chelsea watashindwa
kucheza vyema na Liver walifanikiwa hilo kwa
sehemu kubwa ya mchezo.
7. “SUB” ZA CONTE
Ukiachana na wachezaji 11 ambao Conte
amekuwa akiwatumia mara kwa mara kwa
sehemu kubwa ya mechi za ligi ya primia,
Kwa mchezo wa jana na michezo mingi
iliyopita Conte ameonyesha ubora ktk
kuifanyia timu mabadiliko yanayoleta tija,
ukiangalia mchezo dhidi ya Liver kuingia kwa
Pedro na Fabregas kuliifanya Chelsea ipate
uhai zaidi eneo la mbele. Lakini pia benchi la
Chelsea lina “quality” uifananisha na benchi
la Liver.
8. WILLIAN KUMWEKA BENCHI PEDRO
MMMMMH!
Mchezaji bora ndani ya klabu ya Chelsea kwa
msimu uliopita alikuwa ni Willian na ni katika
msimu ambao yeye pekee ndiyo alionekana
“hana mgomo” dhidi ya kocha Jose Mourinho
ila msimu huu Willian amekuwa na kiwango
cha kawaida mbele ya Pedro, kwa mchezo wa
jana Willian alianza ili kuifanya Chelsea iweze
kucheza kwa umahiri zaidi “counter attacks’
ila hakufanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuingia
kwa Pedro tofauti iliweza kuonekana, Mchezo
unaofuata dhidi ya Arsenal sifikiri kama
Willian atakuwa ndani ya wachezaji 11 wa
kwanza.

MI BINAFSI NIMEONA HAYO  
            By mpenda maboko
                  Wanasoka watakuwa wameelewa

No comments