Breaking News

Julio atoa neno kwa mavugo

Mavugo amemshukuru kocha wa zamani wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo kwa nasaha zake nzuri zilizomrudisha mchezoni, Je Julio alimwambia nini Mavugo?
Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea klabu ya Simba Laudit Mavugo, amemshukuru kocha wa zamani wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo kwa nasaha zake nzuri zilizomrudisha mchezoni.
Mavugo ameiambia nijuzehabari, kabla ya mchezo huo Julio aliongea naye kwa muda mrefu akisisitiza kuwa yeye ni mchezaji mzuri na anauwezo wa kuipa timu hiyo matokeo.
“Ameniambia ni mchezaji ambaye Simba inanitegemea na ubingwa wa msimu huu upo mikononi mwangu, kwa kweli maneno hayo yalinijenga na kunifanya nijiamini muda wote wa mchezo,”amesema Mavugo.
Mshambguliaji huyo aliyefunga bao la mwisho katika mchezo wa jana dhidi ya Majimaji, amesema ataendelea kumuheshimu na kumsikiliza kocha huyo kwasababu anahisi amebadilisha maisha yake ya soka.
Amesema tangu atue Tanzania, hajawahi kupata mtu na kuzungumza naye maneno muhimu kama hayo na kumfanya ajione yeye ni shujaa kwa miambi hiyo ya soka Tanzania.
“Ukweli maneno ya Julio yamenijenga na kujiona jasiri na sasa naamini nitabadilika na kufunga katika kila mechi ambayo nitapangwa kwenye kikosi cha Simba.
Awali mchezaji huyo amesema alijihisi kuwa hana thamani ndani ya klabu hiyo kutokana na kushindwa kufanya vizuri ikiwemo kufunga katika mechi nyingi hata mashabiki wa timu hiyo kutamani atupiwe virago.
Bao la jana limemfanya mshambuliaji huyo ambaye pia huichezea timu ya taifa ya Burundi kufikisha mabao 5, kwenye ligi ya Vodacom, ukiwa ni msimu wake wa kwanza tangu atue msimbazi akitokea Vital’O, ya kwao Burundi.
Katika mchezo huo wa jana kocha Joseph Omog, alibadili utaratibu wake wa kumpumzisha mchezaji huyo na kuamua kumchezesha kwa dakika zote 90, na katika dakika ya 88 ndipo alipofunga bao hilo ambalo liliihakikishia ushindi timu yake na kupunguza gepu la pointi kutoka nne hadi moja

No comments