CARRAGHER: HENRIKH MKHITARYAN NI ZAIDI YA MESUT OZIL
Carragher ameibuka na jipya akidai Henrikh Mkhitaryan ni mchezaji hatari na mwenye kasi zaidi kuliko Ozil, Mata na Silva
Gwiji la Liverpool Jamie Carraher ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka amedai kuwa Henrikh Mkhitaryan ni mchezaji mwenye ubora zaidi ya Mesut Ozil , Silva na Mata.
Akizungumzia kuhusu kiwango alichoonesha mchezaji huyo katika mechi ya Manchester United dhidi ya Leicester City Jamie alisema, “Mhhitaryan ana kitu ambacho wachezaji wachache wa aina yake wanacho.”
Kitu hicho amekitaja kuwa ni kasi thabiti inayofanana muda wote anapokuwa dimbani.
“Utawafikiria watu kama Mata, Ozil na Silva kama watu ambao wana uwezo mkubwa sana kwenye wa kutembea na mpira uwanjani lakini Mkhitaryan yupo kwenye anga nyingine.”
Mkhitaryan alikua ni mmoja kati ya waliofunga magoli kwenye mechi dhidi ya Leicester City.
Je, unadhani Mkhitaryan ana uwezo huo zaidi ya Ozil, Silva na Mata?
Toa maoni yako ni mchezaji gani katika soka la bongo unaweza kumfananisha na nyota wa huyo Manchester United
No comments