Breaking News

ARSENE WENGER KUTAZAMA MCHEZO JUKWAANI DHIDI YA CHELSEA

Wenger atakuwa akitumikia kifungo cha mechi ya tatu kati ya nne Gunners watakapowakabili mahasimu wao wa London
Meneja wa Arsenal , Arsene Wenger imeripotiwa atakaa kwenye jukwaa la mashabiki wa Chelsea katika mechi ya Ligi Jumamosi baina ya timu hizo mbili katika uwanja wa Stamford Bridge.
Wenger atakuwa akitumikia kifungo cha mechi ya tatu kati ya nne Gunners watakapowakabili mahasimu wao wa London. Mpangilio wa uwanja haumruhusu kufungiwa kwenye kizimba.
Mfaransa huyo amepewa kuzungumza na timu kabla ya mechi na kipindi cha mapumziko na pia ni lazima azungumze na vyombo vya habari baada ya mechi, mambo ambayo hayatakuwa rahisi iwapo atafungiwa kwenye kizimba ambacho kipo upande wa magharibi mwa uwanja.
Badala yake, Evening Standard kimeripoti kuwa Wenger atakaa jukwaa la kati upande wa mashariki kwani vyumba vya kubadilishia nguo vipo upande huo wa uwanja.
Wenger atasindikizwa kwenda na kuondoka kitini mwake na walinzi, huku Arsenal nao wakitarajiwa kuleta mlinzi wao kukaa pembeni mwa meneja huyo veterani kipindi chote cha mechi.
Arsenal watasafiri kwenda Darajani Stamford wakijua kwamba kipigo kitawafanya wawe pointi 12 nyuma ya vinara Chelsea.

No comments