Breaking News

CARLO ANCELOTT APATA WAKATI MGUMU JUU YA KIBARUA CHAKE BAADA YA KIPIGO CHA JANA KUTOKA KWA PSG

                               Mwenyekiti wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge amesema matokeo ya timu yake dhidi ya PSG hayakutegemewa na lazima maongezi yafanyike kujadili mstakabali wa kocha Carlo Ancelotti.   
Bayern Munich ikiwa ugenini imepokea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG kwenye mchezo wa pili Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi usiku wa kuamkia leo..
Rummenigge amesema, “Matokeo ya mchezo wa jana hayakutegemewa na siyo matokeo mazuri kwa timu kama Bayern hivyo lazima wakae chini na mwalimu kujadili hilo”.
Bayern iliruhusu bao la mapema kutoka kwa Dan Alves kabla ya Edinson Cavani kuongeza la pili na baadae Neymar kumaliza maangamizi kwa bao la tatu.


No comments