Breaking News

HISTORIA YA BOCA JUNIORS NA MAFANIKIO YAKE

Aprili 3, 1905, ilianzishwa klabu ya soka ya Boca Juniors ya nchini Argentina katika kitongoji cha La Boca karibu na jiji la Buenos Aires. Klabu hiyo ilianzishwa na waitaliano watano waliokuwa wahamiaji nchini humo Esteban Baglieto, Juan Farenga, Teodoro Farenga, Santiago Sana na Alfredo Scarpati.
Mechi ya kwanza kwa miamba hiyo kucheza ilikuwa Aprili 21, 1905. Boca huvaa jezi za rangi ya Bluu na Manjano na iliwahi kuripotiwa kwamba waliiga rangi kutoka bendera ya Sweden.
Awali walikuwa wakitumia jezi zilizokuwa na mistari ya rangi nyeupe na nyeusi ambazo walikuja kuziacha kwani zilikuwa zikifanana na klabu nyingine nchini humo.
Mwaka 1913 Boca Juniors ilipanda daraja ikitokea daraja la kwanza.

Miamba hiyo ilitwaa taji lao la kwanza mwaka 1919 na kuanzia hapo ikaanza kuchukua mfululizo ya ndani ilichukua 31 na 18 ya Kimataifa. Katika medani ya kimataifa wakati inachukua hayo yalikuwamo mataji manne ya FIFA Club World mwaka 1977, 2000, 2003 na 2007.
Pia klabu hiyo imefanikiwa kuwatoa nyota wakali wa dunia, utakuwa ukimkumbuka Juan Roman Riquelme (1995-2002), Carlos Tevez (2001-04) na mkongwe Diego Maradona (1981-82, 1995-97). Pia imekuwa ikijitahidi kuendeleza vipaji huku ikiwatoa wachezaji wakali kama Sebastián Battaglia, Nicolás Burdisso, Éver Banega na Fernando Gago
Boca Juniors inashika nafasi ya tatu duniani kwa kufahamika nyuma ya Real Madrid na AC Milan. Uwanja wao unafahamika Alberto J. Armando maarufu La Bombonera.
Mahasimu wakubwa wao wakubwa ni River Plate kwani zote zilianzishwa hapo La Boca.







No comments